Mke Wa El Chapo Emma Coronel Aispuro Akamatwa Marekani kwa Ulanguzi Wa Mihadarati

 

Mke wa mlanguzi mkuu wa mihadarati kutoka Mexico El Chapo Guzman amekamatwa nchini Marekani kwa tuhuma za ulanguzi wa mihadarati , imesema mamlaka nchini humo.

Emma Coronel Aispuro , mwenye umri wa miaka 31 alikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles nje ya mji mkuu wa Washington DC.

Anashtakiwa kwa kushiriki katika njama ya kutaka kusambaza dawa aina ya Cocaine, Methamphetamine, heroin na bangi.

Guzman kwasasa anahudumia kifungo cha maisha jela mjini New York kwa kuhusika katika ulanguzi wa mihadarati na fedha.

Jamaa huyo mwenye umri wa miaka 63 ni kiongozi wa zamani wa kundi la walanguzi wa mihadarati wa Sinaloa ambalo ndilo lililokuwa na mtandao mkubwa wa usambazaji wa mihadatari nchini Marekani.


EmoticonEmoticon