Rais Joe Biden ameahidi kwamba Marekani itashirikiana na washirika wake wa Ulaya katika juhudi za kukabiliana na changamoto za janga la maambukizi ya corona, ugaidi na mabadiliko ya tabia nchi.
Katika
hotuba yake rais Biden amesisitiza umuhimu wa kuitetea na kuidumisha demokrasia
duniani. Amewaambia viongozi wa nchi tajiri za G7 walioshiriki kwenye mkutano
huo kwamba demokrasia inahujumiwa barani Ulaya na nchini Marekani. Rais Biden
amesema Marekani itajizatiti katika kuuimarisha uhusiano kati yake na nchi za
bara la Ulaya.
Katika
mkutano huo wa Munich wa masuala ya usalama rais huyo wa Marekani alizungumzia
pia juu ya mabadiliko ya tabia nchi. Amesema suala hilo linahusu uhai wa
binadamu wote na kwa ajili hiyo Biden ameirudisha Marekani kwenye mkataba wa
Paris juu ya mabadiliko ya tabia nchi.
Juu ya janga la maambukizi ya corona, Biden amesema ushirikiano wa dunia nzima unahitajika katika juhudi za kukabiliana na janga hilo na ametoa mwito wa kuchukuliwa hatua kabambe. Marekani itatenga kiasi cha dola bilioni 4.5 kwa ajili ya kuunga mkono mpango wa chanjo kwa manufaa ya nchi masikini.
EmoticonEmoticon