Tedros amesema
baadhi ya nchi zenye kipato cha juu zinaingia mikataba na watengenezaji wa
chanjo ambapo inadhoofisha mikataba ambayo COVAX imefanya na kampuni hizo
hizo za kutengeneza madawa
Mkuu wa shirika la afya Duniani-WHO, Tedros Adhanom
Ghebreyesus, Jumatatu amesema baadhi ya mataifa tajiri Duniani yanadumaza
juhudi zinazofanywa na shirika lake na marafiki zake kupata chanjo kwenda
mataifa maskini sana Duniani.
Tedros alishiriki katika mkutano wa pamoja kwa njia ya video
na Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier wakizungumzia kuhusu mpango wa
chanjo ya kimataifa uliowezeshwa na WHO na COVAX uliobuniwa kupata na kusambaza
kwa usawa chanjo za COVID-19 kote Duniani.
Akizungumza
kutoka makao makuu ya WHO mjini Geneva, Tedros amesema baadhi ya nchi zenye
kipato cha juu zinaingia mikataba na watengenezaji wa chanjo ambapo
inadhoofisha mikataba ambayo COVAX imefanya na kampuni hizo hizo ikipunguza
idadi ya dozi ambazo COVAX inaweza kununua.
Hata hivyo Ghebreyesus hakuzitaja nchi hizo. Mkuu huyo wa WHO amesema anahakikisha kuwa kuna chanjo za kutosha huku zikishirikisha mataifa maskini sana duniani ili kusaidia kila mtu.
EmoticonEmoticon