Msaidizi Wa Muigizaji Kevin Hart Ahukumiwa Kwa Kuiba $1m

 

Msaidi wa zamani wa Kevin Hart ameshtakiwa kwa kuiba zaidi ya dola milioni moja '$1m (£730,000) kutoka kwa nyota wa Marekani.

Dylan Jason Syer, ambaye alianza kufanya kazi kama muigizaji wa Jumanji mwaka 2015, anashutumiwa kwa kuthibitisha manunuzi ambayo yalikuwa ayajaidhinishwa kwa kutumia kadi ya Hart.

Anashutumiwa kufanya ulaghai huo wa malipo kati ya mwezi Oktoba 2017 na Februari 2019.

Kijana huyo mwenye miaka 29 ameshtakiwaa kwa madai ya uhalifu wa wizi wa fedha, wizi wa utamblisho na ulaghai.

Kama atakutwa na hatia , bwana Syer, kutoka kisiwa cha Long Island City mjini New York, atahukumiwa miaka 25 gerezani. Mtuhumiwa huyo atarudi mahakamani Februari 17.


EmoticonEmoticon