Polisi na
vikosi vya usalama katika mji mkubwa zaidi nchini Myanmar walifyatua risasi za
kuwaonya waandamanaji Ijumaa.
Risasi hizo zilirushwa wakati vyombo hivyo vya usalama
vilipokuwa vikisogea kuvunja kundi la waandamanaji wapatao elfu moja.
Waandamanaji hao walikuwa wamekusanyika katika jumba maarufu
la maduka katika kitongoji cha Tamwe cha Yangon usiku kupinga afisa
aliyeteuliwa na jeshi.
Waandamanaji walikuwa wakishikilia mabango na wakipiga kelele
wakilaani mapinduzi ya Februari mosi, licha ya kuongezeka kwa uwepo wa vikosi
vya usalama na lori la maji ya kuwasha lililokuwa katika eneo hilo.
Kulingana na
vyombo vya habari vya serikali na mashuhuda kitengo cha karibu polisi 50 wa
kutuliza ghasia walichukua hatua dhidi ya waandamanaji na kumkamata
mwandamanaji mmoja.
Shirika la habari la Reuters linaripoti kuwa mwandishi wa habari wa Kijapani alikamatwa kwenye maandamano huko Yangon Ijumaa. Kama ikithibitishwa, ukamataji huo utakuwa ni wa kwanza kwa mwandishi wa habari wa kigeni tangu mapinduzi.
EmoticonEmoticon