New Zealand Yafunga Shughuli Kufuatia Visa Vya Corona

 

Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern ametangaza vizuizi vya kufunga shughuli kwa siku tatu katika mji mkubwa wa Auckland baada ya kugundulika visa vitatu vya virusi vya corona. 

Hata hivyo visa hivyo visa hivyo bado havijatambuliwa huku baadhi ya mataifa ya Ulaya yakifunga mipaka ili kuzuia kusambaa kwa virusi vinavyobadilika vya coronaWanafunzi wawili Hong Kong waambukizwa kirusi kipya. Hali bado ni tete kufuatia kusambaa zaidi kwa virusi hivyo vipya. 

Baada ya kikao cha dharura na baraza la mawaziri waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern alisema wameamua kuchukua mwelekeo wa tahadhari hadi pale watakapokuwa na taarifa zaidi kuhusu mlipuko huo. 

Visa hivyo vitatu vinahusisha mtu na mke wake pamoja na binti yao na ni vya kwanza kugundulika ndani ya taifa hilo tangu Januari 24.

Vizuizi vya kufunga shughuli vinarejeshwa tena kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi sita nchini New Zealand na kuonekana pigo dhidi ya mafanikio makubwa ya kulidhibiti janga hilo nchini humo.

Alisema, "Kitu kikubwa ninachowaomba watu wa Auckland ni kubaki nyumbani ili kuzuia hatari ya kusambaa. Watu wanatakiwa kufanya kazi kutokea nyumbani, labda tu kama haiwezekani. Kama utatoka nje, tafadhali kaa mbali kwa umbali wa mita mbili ama uko kwenye maeneo yenye usimamizi ambayo unajua kuna  watu wengine, basi ni mita moja."


EmoticonEmoticon