Papa Francis Amemteua Mwanamke Wa Kwanza Kuwa Katibu

Kiongozi wa kanisa katoliki dunia Papa Francis amemchagua mwanamke wa kwanza kuwa katibu katika baraza la mkutano wa maaskofu.

Nathaniel Becquart , ambaye anatoka Ufaransa atakuwa na haki za kupiga kura katika baraza hilo ambalo hutoa ushauri kwa papa na kushiriki katika mijadala inayohusisha masuala tata katika kanisa hilo.

Bi Becquart amefanya kazi katika baraza la mikutano hiyo kama mshauri tangu 2019.

Katibu mkuu wa bodi hiyo , kadinali Mario Grech , alisema kwamba uteuzi huo umeonesha kwamba 'mlango umefunguliwa'.

Amesema kwamba uamuzi huo unaonesha lengo la Papa la kutaka wanawake wengi zaidi kushiriki mchakato wa utambuzi na maamuzi katika kanisa hilo.


EmoticonEmoticon