Polisi
nchini Myanmar katika mji mkuu wa Nay Pyi Taw wametumia maji ya kuwasha dhidi
ya wafanyakazi wanaofanya maandamano kote nchini humo dhidi ya mapinduzi ya
kijeshi.
Maelfu ya raia wanashiriki maandamano kwa siku ya tatu
wakitoa wito wa kuachiwa huru kwa kiongozi mkuu wa nchi hiyo Aung San Suu Kyi
na kurejeshwa kwa demokrasia.
Hatua hiyo inawadia baada ya Myanmar kushuhudia maandamano
makubwa katika kipindi cha zaidi ya miaka kumi.
Wiki iliyopita, jeshi lilipindua serikali ya nchi hiyo baada ya
kudai kwamba uchaguzi uliokuwa umefanyika awali, ulikumbwa na udanganyifu bila
kutoa ushahidi wowote.
Pia jeshi
lilitangaza hali ya tahadhari kwa kipindi cha mwaka mmoja nchini Myanmar ambayo
pia inafahamika kama Burma, na mkuu wa jeshi Min Aung Hlaing amechukua uongozi
wa nchi hiyo.
Bi. Suu Kyi na viongozi waandamizi wa chama cha National League for Democracy (NLD), akiwemo Rais Win Myint, wamewekwa chini ya kizuizi cha nyumbani.
EmoticonEmoticon