Raia Wa Niger Wapiga Kura Kuchagua Rais Mpya

 

Nchini Niger duru ya pili ya uchaguzi wa rais inatarajiwa kuleta mabadiliko ya kidemokrasia kwa mara ya kwanza tangu taifa hilo la Afrika Magharibi lilipopata uhuru wake kutoka kwa Ufaransa mnamo mwaka 1960. 

Mgombea wa chama tawala Mohamed Bazoum anatarajiwa kushinda hasa baada ya kuongoza kwa asilimia 39.3 ya kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa Desemba 27. 

Mpinzani wake ni rais wa zamani wa nchi hiyo Mahamane Ousmane, ambaye kwenye duru ya kwnza alipata asilimia 17% ya kura.

Bazoum, mwenye umri wa miaka 61 ambaye aliwahi kushika nafasi kadhaa za juu pamoja na wizara za mambo ya nje na mambo ya ndani katika serikali inayomaliza muda wake ya rais Mahamadou Issoufou anaungwa mkono na wagombea walioshika nafasi za tatu na wa nne katika duru ya kwanza ya uchaguzi.


EmoticonEmoticon