Rais wa Marekani Amesema Yuko Tayari Kujenga Upya Mahusiano Na Umoja Wa Afrika

 

Rais wa Marekani Joe Biden ameahidi kujenga upya ushirika wa nchi hiyo na Umoja wa Afrika (AU) muda mchache baada ya kutoa hotuba ya kwanza kuhusu sera za mambo ya nje tangu kuingia madarakani.

Mtangulizi wake, Donald Trump, alizusha mgogoro mwaka 2018 kwa madai ya kutumia neno ''chafu'' kuelezea mataifa ya Afrika. Bwana Trump baadae alikana madai kuwa yeye ni mbaguzi wa rangi.

Siku ya Ijumaa Ikulu ya White House ilitweet video ya matamshi ya Rais Biden kuhusu bara hilo kabla ya mkutano wake wa 34. Alisema: ''Utawala wangu unajitoa kujenga tena ushirika wetu duniani na kujihusisha tena na taasisi za kimataifa kama vile Umoja wa Afrika.

''Pia lazima tukabiliane na changamoto kubwa zilizopo. Hiyo ni pamoja na kuwekeza zaidi katika afya ya ulimwenguni, kuishinda Covid-19 na kufanya kazi ya kuzuia, kugundua na kushughulikia shida za kiafya za siku zijazo, na kushirikiana na kituo cha kupambana na magonjwa cha Afrika CDC na taasisi zingine kuendeleza usalama wa afya. " Alisema Biden. 


EmoticonEmoticon