Rais Wa Marekani Joe Biden Awania Kulifunga Gereza La Guantanamo Bay

 

Rais wa Marekani Joe Biden anataka kulifunga gereza la Guantanamo Bay linalotumiwa kuwashikilia washukiwa wa ugaidi. Biden antaka kulifunga gereza hilo kabla ya muhula wake kumalizika. 

Hatua hiyo ya rais Biden ni katika muendelezo wa kuitimiza ahadi ya utawala wa Barack Obama ya kuifunga jela hiyo yenye utata. Obama mnamo mwaka 2016 alisema kuiendesha mahabusu hiyo haikuwa tu ni sera mbaya bali pia ni njia mojawapo ya kupoteza pesa, kwa sababu inagharimu zaidi ya dola milioni 445 kwa mwaka.

Wasaidizi wa Rais Joe Biden wameanza kulingalia upya swala la owepo wa jela hiyo ya Guantanamo Bay na wameanzisha majadiliano ya ndani yanayozingatia hatua ya kiutendaji itakayosainiwa na rais Biden katika wiki au miezi ijayo. 

Hayo yanaashiria juhudi mpya za kuondoa kile watetezi wa haki za binadamu wanachokiita kuwa ni jambo linaloitia doa Marekani kwenye sura ya ulimwengu.

Alipoulizwa katika mkutano na waandishi wa habari juu ya uwezekano wa kufungwa kwa gereza hilo lililopo nchini Cuba msemaji wa ikulu Jen Psaki amesema ni kweli hilo ni lengo na nia ya utawala wa rais Joe Biden.


EmoticonEmoticon