Rais Wa Somalia Hatakiwi Kushiriki Mazungumzo Yeyote Ya Kutatua Mzozo Nchini Humo

Muhula wake kuwepo madarakani uliisha mwanzoni mwa Februari na bunge lilipanga kufanya uchaguzi Februari 8 ukacheleweshwa kwa sababu wabunge wapya bado hawajachaguliwa huku upinzani unamshutumu Farmajo kujaza wafuasi wake katika bodi ambazo huchagua wabunge

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed maarufu Farmajo ambaye muhula wake wa miaka minne madarakani ulifikia kikomo mwanzoni mwa mwezi huu hatakiwi kushiriki katika mazungumzo yanayolenga kutatua mzozo ambao umechelewesha kufanyika uchaguzi mkuu mpya wa nchi hiyo, serikali za majimbo mawili kati ya matano nchini Somalia zimesema Jumapili.


EmoticonEmoticon