Rais Biden
anatoa wito wa kupitishwa haraka pendekezo lake la mfuko wa auheni ya msaada wa
dola trilioni 1.9 za virusi vya Corona unaojumuisha hundi huku akiweka
kando wito uliotolewa na maseneta wa Republican kwa mpango mdogo zaidi wa dola
bilioni 618
Rais wa Marekani Joe Biden amerudia tena nia yake ya kutuma msaada wa dola 1,400 kwa mamilioni ya wamarekani watu wazima ili kuinua uchumi wa nchi ulioharibika kutokana na janga la virusi vya Corona.
Lakini anasema
anakaribisha maoni kufuatia madai ya waRepublican kuongeza masharti juu ya nani
atapata fedha hizo.
Akitoa hotuba kwa wabunge wa Democratic katika baraza la
wawakilishi na baadae kwenye mkutano wa kundi la maseneta wa Democratic, Rais
Biden alitoa wito wa kupitishwa haraka pendekezo lake la mfuko wa auheni ya
msaada wa dola trilioni 1.9 za virusi vya Corona ambao unajumuisha hundi huku
akiweka kando wito uliotolewa na baadhi ya maseneta wa Republican kwa mpango
mdogo zaidi wa dola bilioni 618.
Rais Biden
amewaambia wabunge kwamba yupo tayari kuweka kikomo cha mapato ya chini juu ya
nani atapata hundi za dola 1,400 lakini sio kupunguza ukubwa wa malipo.
Sambamba na malipo ya dola 600 yaliyoidhinishwa na Rais wa zamani Donald Trump mwezi Disemba mwaka jana, msaada wa dola 2,000 kwa pamoja utakuwa sawa na ahadi ya Biden aliyotoa wakati wa kampeni yake ya ushindi kwa White House mwaka 2020.
EmoticonEmoticon