Raisi Wa Marekani Amesema Idadi Ya Vifo 500,000 Marekani Ni Hatua Ya Kuumiza Sana

 

Rais wa Marekani, Joe Biden amehutubia taifa baada ya kurekodi vifo 500,000 vilivyotokana na virusi vya corona, idadi kubwa zaidi kufikiwa ulimwenguni.

''Kama taifa, hatuwezi kukubali mwisho huu mbaya. Tunapaswa kuepuka kufa ganzi kwa huzuni,'' alisema.

Rais na Makamu wa Rais , na wake zao, kisha walikaa kimya nje ya White House wakati wa tukio la kuwasha mshumaa.

Zaidi ya Wamarekani milioni 28.1 wamepata maambukizi ambayo pia ni idadi ya juu zaidi duniani.

“Leo ninawaomba Wamarekani kukumbuka. Kukumbuka wale tuliowapoteza na kuwakumbuka tuliowaacha,''

"Mara nyingi tunasikia watu wakielezewa kama Wamarekani wa kawaida," aliendelea kusema. "Hakuna kitu kama hicho, hakuna kitu cha kawaida juu yao. Watu tuliopoteza walikuwa zaidi ya watu wa kawaida . Walikuza vizazi. Walizaliwa Marekani, walihamia Marekani."

"Wengi wao walivuta pumzi yao ya mwisho wakiwa peke yao Marekani," aliendelea. Kwangu mimi, kupambana na huzuni na uchungu ni kulitafuta kusudi,'' alisema.

Rais Biden alisema akiwataka Wamarekani kupambana na Covid-19 kwa pamoja.


EmoticonEmoticon