Raisi Wa Marekani Asaini Agizo Kubadili Sera Ya Familia Za Wahamiaji Kutenganishwa Na Watoto Wao

 

Rais wa Marekani Joe Biden amesaini maagizo matatu ya rais ya kuunganisha familia za wahamiaji zilizotenganishwa kutokana na sera ya utawala wa Trump na pia anataka kupitia tena ajenda yote ya uhamiaji kwa ukubwa zaidi.

Katika jaribio lake la kuzuia uhamiaji haramu, utawala wa Rais Donald Trump ulitenganisha watu wazima ambao hawakuwa na stakabadhi sahihi za uhamisho halali na watoto wao wakati wanavuka mpaka wa Marekani na Mexico.

Maagizo ya Bwana Biden yataanza kwa kuanzisha jopo kujaribu kuunganisha watoto wanaokadiriwa kuwa kati ya 600 na 700 ambao bado wametengana na familia zao.

Utawala wa Trump ulitenganisha watoto karibu 5,500 na wazazi wao ama waangalizi wao katika mpaka huo mwaka 2017-2018.


EmoticonEmoticon