Raisi Wa Marekani Azungumza Na Benjamin Netanyahu

 

Rais Joe Biden wa Marekani amezungumza kwa simu na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ikiwa ni mara ya kwanza kwa viongozi hao na kujadiliana kuhusu ushirikiano baina ya mataifa yao. 

Rais Joe Biden wa Marekani amezungumza kwa simu na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ikiwa ni mara ya kwanza kwa viongozi hao na kujadiliana kuhusu ushirikiano. 

Miongoni mwa masuala yaliyotiliwa umuhimu ni ushirikiano baina ya mataifa hayo na amani katika eneo la Mashariki ya Kati, hususan baina ya Israel na Palestina. 

Hata hivyo mazungumzo hayo hayakuonekana kuwa ya kawaida baada ya kusogezwa mbele kwa takriban mwezi mmoja, tofauti na huko nyuma ambapo viongozi wa mataifa hayo huzungumza katika kipindi cha siku chache baada ya kuingia madarakani.

Kusogezwa mbele kwa mazungumzo hayo kuliibua madai kwamba Biden alikuwa akikwepa kuzungumza na Netanyahu, na hasa kutokana na ukaribu aliokuwa nao waziri mkuu huyo na mtangulizi wa Biden, Donald Trump. 

Mapema wiki hii, msemaji wa ikulu ya White House Jen Psaki aliwaambia waandishi wa habari kwamba mazungumzo hayo yangali karibu mno.

Alisema, "Ngoja nianze kwa kuwathibitishia kwamba simu yake ya kwanza na viongozi wa kikanda ni ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu. Itakuwa hivi karibuni. Mnajua, Israel ni mshirika wetu."


EmoticonEmoticon