Raisi Wa Marekani Kuwakumbuka Wahanga 500,000 Wa COVID-19

 

Rais Joe Biden wa Marekani hii leo ataungana na raia nchini humo kuwakumbuka watu 500,000 waliofariki dunia kutokana na janga la virusi vya corona, kwa kukaa kimya na kuwasha mishumaa katika hafla itakayofanyika Ikulu ya White House.

Idadi ya vifo nchini Marekani inahofiwa kuwa itavuka kiwango hicho cha kutisha hii leo, ikiwa ni mwaka mmoja tu baada ya kugundulika mtu wa kwanza aliyeambukizwa COVID-19 nchini humo. 

Ikulu ya White House imesema Biden atatoa hotuba nyakati za jioni kukumbuka maisha ya watu yaliyopotea. Ataungana na mke wake, Jill Biden, na Makamu wa Rais Kamala Harris pamoja na mumewe, Doug Emhoff.

Rais Biden amelifanya suala la vita dhidi ya virusi vya corona kuwa sehemu muhimu ya utawala wake, akijitenganisha na jinsi mtangulizi wake, Donald Trump, alivyolishughulikia janga hilo la kilimwengu.


EmoticonEmoticon