Rais wa
Uganda Yoweri Museveni ametangaza kuwa shule zitafunguliwa mwezi Machi kwa
wanafunzi waliobakisha mwaka mmoja kuhitimu masomo yao.
Huku Wanafunzi wa madarasa mengine
watasubiri mpaka baada serikali kupata chanjo ya virusi vya corona mwezi wa
Aprili mwaka huu.
Rais Museveni amesema wanafunzi wa
darasa la sita , kidato cha tatu na kidato cha tano wataungana na wenzao
watahiniwa tarehe mosi mwezi wa Machi mwaka huu kuanza masomo.
Hii ni karibu mwaka mmoja tangu Rais
Museveni alipotangaza kufungwa shule mwaka jana tarehe 20 Machi 2021, wakati
Uganda ilipochukuwa tahadhari za kuzui maambukizi ya virusi vya corona.
Museveni amesema wanafungua shule kwa
madarasa hayo baada ya uchunguzi uliofanywa na wanasansi na kukuta idadi hiyo
ni ndogo ukiliganisha na wanafunzi wa madaraka yote nchini Uganda ambao ni kama
milioni 15.
Baadhi ya walimu wanaomba serikali
kuwaruhusu wanafunzi wote warudi shuleni kwani hata huko nyumbani hawako salama
kwa kujikinga maambukizi ya virusi vya corona.
Hata hivyo Rais Museveni alieleza pia
Uganda inatarajia kupata chanjo ya virusi vya corana mwezi wa Aprili mwaka huu
hivyo baada ya kupata chanjo hiyo madarasa mengine yatafunguliwa.
Lakini vyuo vitafungua kuanzia mwezi ujao pia.
EmoticonEmoticon