Rapa Bobby Shmurd amekuwa nyumbani kwa siku
chache tu tangu aachiliwe kutoka gerezani Februari 23, lakini hakika amekuwa
akihisi upendo tangu kuachiliwa kwake ambapo alikaribishwa nyumbani na mikono
miwili na wapendwa wake,
Katika mahojiano yake na GQ siku
yake ya kwanza akiwa nje, Bobby ameelezea safari yake akiwa gereza hadi sasa
aliporudi nyumbani, Bobby Shmurda anasema hana mpango wa kuwa nyuma ya nondo
tena baada ya kusota gerezani kwa zaidi ya miaka mitano,
"Nimemaliza na hiyo jela,"
alisema Bobby na kusisisitiza kuwa amejifunza na hategemei kurudia kufanya
makosa yaliyopelekea kuwa mbali na wapendwa wake kwa kipindi chote hicho.
Rapa huyo Mzaliwa wa Miami alifungwa
jela tangu mwaka 2014 akishtakiwa kwa makosa kadhaa ikiwemo kula njama ya
kufanya mauaji, Biashara za dawa za kulevya na umiliki wa Silaha kinyume cha
sheria.
EmoticonEmoticon