Rwanda imeanza zoezi la kutoa chanjo ya virusi vya corona kwa wananchi wake wiki moja baada ya wakazi wa mji mkuu wa nchi hiyo Kigali kuondoka katika zuio la kukaa ndani.
Zoezi la kuitoa chanjo
hiyo limetangazwa kwa umma na wizara ya afya nchini Rwanda na imeanzia
kutolewa kwa makundi yaliyo katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa wa COVID-19.
Hata hivyo, wizara hiyo haikutangaza ni kiasi gani cha chanjo inayotolewa na idadi
ya watu wanaotakiwa kuchanjwa kwa muda fulani.
Lakini
imesema kwamba watu wenye hatari ya kupata maambukizi kwa urahisi ndiyo
wameanza kuchanjwa kama vile wahudumu wa afya pamoja na wafanyakazi wote
walioko kwenye sekta ya afya hasa wale wanaowahudumia wagonjwa wa virusi vya
corona.
Waziri wa Afya wa Rwanda, Dokta Daniel Ngamije kupitia ukurasa wake wa Twitter amethibitisha kutolewa kwa chanjo hiyo, lakini alijizuia kutoa majibu mwa maswali haya yote.
EmoticonEmoticon