Katika
taarifa iliyotolewa Jumapili, Mahamat alisema uamuzi huo unakomesha
ucheleweshwaji wa kuanzisha mahakama, haki ya mpito, uwajibikaji, maridhiano na
taasisi za kuponya ili kuleta haki na uponyaji kwa wa-Sudan Kusini wote
Mwenyekiti wa kamisheni ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki
Mahamat, anasema anakaribisha uamuzi wa serikali ya mpito ya umoja wa Kitaifa
ya Sudan Kusini wa kuanzisha mahakama ya mseto ya AU kwa nchi hiyo Kama
ilivyotakiwa kwenye makubaliano ya amani yaliyotiwa saini mwaka 2018.
Huku kukiwa na ripoti za ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu
baada ya mzozo kuzuka mwaka 2013 nchini Sudan Kusini, Umoja wa Afrika uliamuru
kuundwa kwa tume ya uchunguzi iliyoongozwa na Rais wa zamani wa Nigeria,
Olusegun Obasanjo. Ripoti ya mwisho ya tume hiyo iliwasilishwa Oktoba mwaka
2015.
Katika taarifa iliyotolewa Jumapili, Mahamat alisema uamuzi huo unakomesha ucheleweshwaji wa kuanzisha mahakama, haki ya mpito, uwajibikaji, maridhiano na taasisi za kuponya ili kuleta haki na uponyaji kwa wa-Sudan Kusini wote.
Wakati huo huo, Nyagoah Tut Put, mtafiti wa haki za binadamu kwa Sudan Kusini anasema hatua iliyofanywa na serikali ya Sudan Kusini inapaswa kutazamwa kwa tahadhari.
EmoticonEmoticon