Shirika la
Afya Dunia (WHO) limeonya dhidi ya maamuzi ya haraka kuhusu ufanisi wa chanjo
ya kukabiliana na virusi vya corona.
Hii ni baada ya utafiti uliofanywa
Afrika Kusini kuonesha kuwa chanjo ya AstraZeneca haitakuwa na ufanisi mkubwa
dhidi ya virusi vipya vya corona vilivyokumba nchi hiyo.
Lakini wataalamu wana matumaini kuwa
chanjo hiyo bado itakuwa na ufanisi katika kuzuia maambukizi makali.
Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom
Ghebreyesus, amesema kuwa data iliyotumiwa kwenye utafiti huo, ilikuwa ni
"majaribio ya watu kidogo tu" na walioshirikishwa walikuwa
"vijana wenye afya zao".
"Ni muhimu kubaini ikiwa chanjo
hiyo ina ufanisi au la katika kuzuia watu kuwa wagonjwa zaidi," amesema
katika taarifa.
Lakini pia ametambua kuwa
watengenezaji wa chanjo watahitajika kuiboresha ili kukabiliana na virusi
hivyo.
"Ni wazi kwamba watengenezaji wa
chanjo watalazimika kuiimarisha zaidi ili kwendana na virusi vipya, hasa
uzingatia virusi vya sasa kwa ajili ya siku za baadaye.
"Tunajua virusi hubadilika na tunajua tunastahili kuwa tayari kuboresha chanjo ili ziendelee kuwa na ufanisi," amesema.
EmoticonEmoticon