Shirika la
afya dunaini limeshauri matumizi ya chanjo ya virusi vya corona iliyotengenezwa
na Chuo Kikuu cha Oxford na AstraZeneca hata kama nchi zinakabiliana na aina
mpya za virusi vya corona.
Baadhi ya aina za virusi hivyo zinaonekana kuifanya aina hiyo
ya chanjo kutokuwa na ufanisi wa kutosha wa kuzuia maambukizi.
WHO pia inasema chanjo hiyo inaweza kutumiwa kwa watu wenye
umri wa zaidi ya miaka 65, jambo linalozuiwa na baadhi ya nchi.
Kutenganisha muda wa utoaji wa dozi za chanjo hiyo, kama
inavyofanyika nchini Uingereza, kunaifanya chanjo hiyo kuwa na ufanisi zaidi,
inashauri WHO.
Chanjo ya
Oxford vinaonekana kama "chanjo ya dunia " kuutokana na kwamba ni
nafuu, inaweza kutengenezwa kwa wingi , na inaweza kutunzwa katika friji ya
kawaida.
Hatahivyo, imeibua utata juu ya ufanisi wake, wengi
wakijiuzliza iwapo inapaswa kutumiwa miongoni mwa wazee na ni kwa muda gani
dozi mbili zinapaswa kutulewa, kutokana na ukosefu wa taarifa(data) kuhusiana
na hilo.
Kikundi cha wataalamu na washauri wa mkakati wa utoaji chanjo wa cha WHO, kinachofahamika kama Sage, kimekuwa kikichunguza kwa kina ushahidi kutoka katika majaribio ya chanjo. Ushauri wake kwa sasa unasema chanjo ya Oxford ina una ufanisi kwa 63%.
EmoticonEmoticon