Maafisa 27 wa Ikulu ya Sudan Kusini
wamethibitihswa kuambukizwa Corona Virus ambapo wamelazimika kuwekwa karantini.
Msemaji wa Ikulu, Ateny Wek Ateny, amesema pamoja na yeye
mwenyewe, walioambukizwa wanatumikia Idara za ulinzi pamoja na huduma za
mapishi na udereva.
Imeelezwa Rais Salva Kiir yupo salama lakini kuanzia sasa
Serikali itadhibiti idadi ya watu wanaopaswa kukutana naye. Pia, atafanya kazi
akiwa nyumbani ili kuepuka maambukizi.
Kwa mujibu wa takwimu za WHO, Sudan Kusini imerekodi visa
6,417 na vifo 85 vya COVID-19 huku waliopona wakiwa 4,014.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon