Wanasayansi
hao wametembelea soko la samaki la Huanan ambalo lilihusishwa na kesi za
COVID-19 na angalau moja ya hospitali huko Wuhan ambayo ilitoa huduma
kwa baadhi ya wagonjwa wa kwanza wa Corona. COVID-19 ni ugonjwa unaosababishwa
na virusi vya Corona
Timu ya wanasayansi wa shirika la afya Duniani-WHO
inayochunguza chanzo cha virusi vya Corona ambacho kiliibuka kwa mara ya kwanza
katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019 wametembelea Jumatatu
kituo cha kudhibiti magonjwa mkoani humo ambacho kilikuwa na jukumu muhimu
katika usimamizi wa mlipuko huo.
China haikutoa maelezo yeyote kuhusu ziara ya timu hiyo
kwenda kituo cha kudhibiti magonjwa cha mkoa wa Hubei. Mmoja wa wanasayansi
katika timu hiyo Peter Daszak amewaambia waandishi wa habari kuwa mkutano
ulikuwa mzuri na uliozaa matunda.
Tangu timu ya WHO ilipowasili mwezi uliopita wanasayansi hao pia wametembelea soko la samaki la Huanan, ambalo lilihusishwa na kesi za COVID-19 na angalau moja ya hospitali huko Wuhan ambayo ilitoa huduma kwa baadhi ya wagonjwa wa kwanza wa Corona. COVID-19 ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona.
EmoticonEmoticon