Spika wa
bunge la Marekani Nancy Pelosi amesema bunge litaanzisha tume huru ya uchunguzi
wa shambulio la Januari 06 katika jengo la bunge la Capitol, lililotekelezwa na
wafuasi wa Donald Trump.
Katika barua hiyo ya wabunge, alisema tume hiyo itafanya
uchunguzi mfano wa tukio la shambulio la Septemba 11 la mwaka 2001 lililotokea
New York na Pentagon.
"Lazima tupate ukweli wa kile kilichotokea ,"
alisema.
Rais wa zamani wa Marekani Trump aliondolewa madai ya
kuchochea ghasia na bunge la seneti.
Lakini
Democrats na baadhi ya Republicans wanaunga mkono jitihada hizo za kufanyika
kwa uchunguzi huru kuhusu ghasia ziizosababisha vifo vya watu watano.
Bi Pelosi amesema luteni jenerali wa jeshi la Marekani Russel
Honoré kwa wiki zilizopita amekuwa akichunguza nini kinahitajika katika
kuimarisha usalama wa eneo la Capitol baada kutokea kwa shambulio hilo.
"Ni wazi kutokana na uchunguzi wake na kesi ya kutokuwa
na imani kwamba lazima ukweli wa kilichotokea ubainike," amesema.
Tume hiyo imesema , "tutachunguza na kuripoti ukweli na
sababu ya kutokea kwa shambulizi; "kuvuruga utaratibu wa kukabidhiana
madaraka kwa amani"; na utayari na vile polisi ilivyoshughulikia
shambulizi la Capitol na wengine wanaohusika katika tekelezaji wa sheria.
Amesema kutokana na ripoti ya awali ya Luteni jenerali Honoré', bunge linahitaji kupata ufadhili wa ziada ili kuweza kuhakikisha usalama kwa wajumbe wake na usalama wa Capitol".
EmoticonEmoticon