Kikosi kazi
cha Muungano wa Afrika (AU) kimesema kuwa Urusi imetoa dozi milioni 300 za
chanjo yake ya Sputnik V COVID-19 pamoja na msaada wa kifedha kwa nchi
zinazotaka kupata chanjo hiyo.
Chanjo ya Urusi inatarajiwa kupatikana kwa kipindi cha miezi
12 kuazia mwezi Mei 2021, AU imesema katika taarifa yake.
Mfuko wa Urusi wa uwekezaji wa moja kwa moja (RDIF), ambao
unahusika na utafutaji wa masoko ya nje, umesema usambaziji wa chanjo hiyo
unaweza kuanza mwezi Mei, zaidi ni kuanzia mwezi Juni.
Nchi 55 wanachama wa Muungano wa Afrika zinatumai kushuhudia 60% ya wakazi wake bilioni 1.3 wanachanjwa kwa kipindi cha trakriban miaka mitatu ijayo.
EmoticonEmoticon