Viongozi Wa G7 Kujadili Juu Ya Chanjo Za COVID-19, Uchumi Na China

 

Rais wa Marekani Joe Biden leo atahudhuria mkutano wa kwanza wa kimataifa tangu aingie madarakani ambapo atashiriki kwenye mkutano wa kilele wa viongozi wa nchi za G7.

Uingereza ni mwenyekiti wa zamu. Msemaji wa ikulu ya Marekani Jen Psaki  amethibitisha kwamba Rais wa Marekani Joe Biden leo atashiriki kwenye mkutano wa kilele  wa G-7 na kwamba ataweka mkazo juu ya hatua za pamoja za dunia nzima katika kupambana na maambukizi ya virusi vya corona, pamoja na utengenezaji na ugavi wa chanjo ya COVID-19  na njia za kufungua uchumi wa dunia ulioathirika vibaya kutokana na janga hilo. 

Psaki amesema Marekani imeahidi kujiunga na mpango wa COVAX, unaohusika na utengenezaji na ugavi wa chanjo kwa nchi zinazoendelea.


EmoticonEmoticon