Wizara ya
mawasiliano na habari ya Myanmar imesema Facebook itazuiwa huduma zake hadi
Februari 7 kwa ajili ya kuweka hali ya utulivu nchini humo. Pia huduma nyingine
zilizozuiliwa ni Messenger, Instagram na WhatsApp
Watoa huduma ya mtandao nchini Myanmar ikiwemo kampuni ya
mawasiliano ya MPT inayomilikiwa na serikali wamezuiwa fursa ya huduma
zinazomilikiwa na kampuni ya Facebook nchini humo siku ya Alhamis kwa saa za
huko, siku kadhaa baada ya viongozi wa jeshi kuchukua madaraka katika njia ya
mapinduzi.
Barua iliyochapishwa mtandaoni na wizara ya mawasiliano na habari nchini humo imesema Facebook itazuiwa huduma zake hadi Februari 7 kwa ajili ya kuweka hali ya utulivu nchini humo.
Baadhi ya watumiaji wa huduma za
mtandao huko Myanmar wanaripoti hawakuweza kupata fursa kadhaa za huduma
zinazotolewa na Facebook.
Kundi
linalofuatilia masuala ya mtandao la NetBlocks, linathibitisha kampuni ya
mawasiliano ya MPT inayomilikiwa na serikali ambayo inasema ina watumiaji
milioni 23, ilizuia mawasiliano ya Facebook pamoja na huduma nyingine kama vile
Messenger, Instagram na WhatsApp.
Kampuni ya Telenor Asa ya Norway ilisema iliizuia Facebook tu kufuatia agizo hilo. Msemaji wa Facebook, Andy Stone anakiri kuwepo hitilafu hizo.
EmoticonEmoticon