Wanademocrat Wataka Trump Atiwe Hatiani Vingenevyo Vitendo Hivyo Vitatokea Tena

 

Wanademocrat wamehitimisha hoja zao kwamba Donald Trump alichochea ghasia za Capitol tarehe 6 mwezi Januari, wakionya "anaweza kufanya hivyo tena" ikiwa hatatiwa hatiani.

Waendesha mashtaka siku ya Alhamisi walitumia maneno ya waandamanaji kumunganisha Bw Trump na vurugu hizo huku wakisema kuwa vurugu hizo ilisababisha madhara ya muda mrefu pia.

Wanademocrat pia waliwasilisha ushahidi kutoka kwa polisi, wafanyakazi, maafisa wa ujasusi na vyimbo vya habari vya kigeni. Timu ya ulinzi ya rais wa zamani itawasilisha hoja zao Ijumaa.


EmoticonEmoticon