Wanasheria Wa Navalny Kukata Rufaa Dhidi Hukumu Ya Zaidi Ya Miaka Mitatu Jela

 

Wanasheriawa kiongozi wa upinzani Urusi, Alexei Navalny, wamesema watakata rufaa kupinga adhabu ya kifungo cha miaka mitatu na nusu jela aliyohukumiwa mpinzani huyo. 

Mahakama imesema Navalny alivunja sheria kwasababu hakuwa akiripoti katika mamlaka ya magereza kama ilivyotakiwa, wakati alipokuwa Ujerumani kwa matibabu baada ya kupewa sumu. 

Tangu mwaka 2014, Navalny amekuwa akikabiliwa na kesi ya madai ya udanganyifu iliyokuwa imesimamishwa kwa muda na ambayo amesema imechochewa kisiasa. 

Kulingana na mawakili wake, huenda Navalny akatumikia kifungo cha miaka miwili na miezi minane kwa vile alishawahi pia kutumikia kifungo cha nyumbani siku za nyuma. Olga Mikhailova, ni mmoja wa mawakili wake:

Kabla ya kutolewa hukumu hiyo na mahakama, Navalny alijitetea kwamba asingeweza kuripoti katika mamlaka ya magereza kama alivyotakiwa kisheria kwani alipoteza fahamu wakati akipelekwa Ujerumani kwa matibabu.

"Nilikuwa nikipatiwa matibabu Ujerumani," amesema Navalny akiwa mahakamani.

Lakini Jaji alisistiza kwamba alilazimika kutimiza masharti hayo katika hali yoyote ile.

"Mahakama imeamua kuunga mkono hoja ya Mamlaka ya Wafungwa," alisema jaji Natalya Repnikova wakati alitangaza uamuzi wa mahakama.


EmoticonEmoticon