Wasichana Zaidi Ya 300 Watekwa Nigeria

 

Wasichana zaidi ya 300 wa shule ya sekondari, wametekwa nyara Februari 25, 2021,  na wanaume waliokuwa na silaha ambao hadi sasa bado hawajajulikana kaskazini magharibi mwa Nigeria jimbo la Zamfara, polisi imesema.

Maafisa wa usalama wamepelekwa katika mji wa Jangebe ambapo wasichana walichukuliwa na kundi la wanaume hao mapema  Ijumaa, polisi wa eneo wamethibitisha utekaji nyara huo lakini hawakutoa taarifa zaidi.

Hii ni idadi kubwa tangu mwaka 2014 ambapo wasichana shule 276 walitekwa nyara kaskazini-mashariki mwa Chibok na wanamgambo wa Kiislamu wa kundi la Boko Haram.

Matukio ya utekaji yameshamiri hivi karibuni, na mara nyingi magenge ya uhalifu huteka nyara wanafunzi wa shule ili kupewa fidia.

Takriban watu 42 wakiwemo wanafunzi 27 walitekwa nyara wiki iliyopita katika eneo la Kagara jimbo jirani la Niger na bado hawajaachiwa.


EmoticonEmoticon