Watumiaji wa
mtandao wa WhatsApp ambao hawatafuata masharti mapya na vigezo mpaka kufikia
tarehe 15 mwezi Mei hawataweza kupokea au kutuma ujumbe mpaka wakubali masharti
hayo.
Akaunti zao zitaorodheshwa kama ''zisizofanya kazi''. Na
akaunti zisizofanya kazi zinaweza kufutwa baada ya siku 120.
Simu na ujumbe wa arifa utafanya kazi kwa ''muda mfupi'' lakini TechCrunch imeripoti, labda kwa ''wiki chache''. WhatsApp ilitangaza mabadiliko mwezi Januari.
Kulikuwa na
mapingamizi miongoni mwa watumiaji ambao walidhani ilimaanisha kuwa kampuni
ilikuwa ikipanga kubadili kiasi cha data inazotoa kwa kampuni mama, Facebook.
Baadaye ilifafanua hii haikuwa hivyo - isipokuwa inalenga
kuwezesha malipo kufanywa kwa wafanyabiashara.
Kuwajulisha watumiaji
WhatsApp tayari inatoa taarifa inshirikisha taarifa kwa
Facebook, kama vile anuani ya IP (nambari zinazoambatanishwa kwenye kila kifaa
kinachojiunga na intaneti, inaweza pia kutumika ili kufahamu mahali kifaa hicho
kilipo) na kufanya manunuzi kutumia jukwaa hilo.
Lakini hali haiku hivyo Ulaya na Uingereza, ambako kuna
sheria za faragha.
Kufuatia tangazo la awali, majukwaa kama Telegram na Signal
yalishuhudia kuongezeka kwa mahitaji, watumiaji wa WhatsApp wakitafuta huduma
mbadala za kutuma ujumbe.
WhatsApp ilichelewesha uchapishaji wa awali na sasa imebadilisha jinsi inavyowarifu watumiaji mabadiliko hayo.
EmoticonEmoticon