WHO Yakutana Na Mameneja, Wakaazi Wa Wuhan

 

Wachunguzi wa Shirika la Afya Duniani - WHO wanaotafuta chimbuko la virusi vya corona mjini Wuhan wamesema upande wa China umewapa kiwango kikubwa cha ushirikiano lakini wametahadharisha dhidi ya kutarajia matokeo ya haraka kutokana na ziara yao.

Pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Virusi ya Wuhan, timu hiyo ya WHO inayojumuisha watalaamu kutoka mataifa 10 wametembelea hospitali, taasisi za utafiti na soko la jadi la wanyama linalohusishwa na mripuko huo.

Mtalaamu wa wanyama Peter Daszak, ambaye ni mjumbe wa timu hiyo ameipongeza mikutano iliyofanywa na wafanyakazi wa taasisi ya Wuhan, ikiwemo na naibu mkurugenzi mkuu aliyeshirikiana na Daszak kuchunguza chimbuko la homa kali ya SARS ambayo ilianzia China na kusababisha mrupuko wa mwaka wa 2003.


EmoticonEmoticon