Aliyekuwa Mke Wa Mtu Tajiri Ulimwenguni Aolewa Na Mwalimu

Bilionea MacKenzie Scott, mtalaka wa mwanzililishi wa Amazon Jeff Bezoz ameolewa na mwalimu wa sayansi katika shule ya watoto wake .

Bi Scott ni mmoja wa wanawake tajiri zaidi duniani na amepeana zaidi ya dola bilioni nne ya mali yake.

Taarifa ya kuolewa kwake na Dan Jewett ilifichuliwa kupitia tovuti ya kutoa misaada.

‘’Dan ni mtu mzuri, nawatakia kila la heri,’’ Bwana Bezos alisema katika taarifa.

Bi Scott, ambaye thamani ya utajiri wake ni karibu dola bilioni 53 kulingana na makadirio ya hivi karibuni ya Forbes,amesema nia yake ni kupeana sehemu kubwa ya mali hiyo.


EmoticonEmoticon