COVID-19 : Maambukizi Duniani Yafikia Milioni 116

Kituo cha kufuatilia maambukizi ya virusi vya Corona cha Johns Hopkins kimerekodi maambukizi zaidi ya milioni 116 ya virusi vya corona duniani.

Kituo cha kufuatilia maambukizi ya virusi vya Corona cha Johns Hopkins kimerekodi maambukizi zaidi ya milioni 116 ya virusi vya corona duniani.

Marekani inaelekea kufikia maambukizi milioni 30, ikifuatiwa na India yenye maambukizi milioni 11 na Brazil milioni 10.8.

Mapema wiki hii, Rais wa Brazili Jair Bolsonaro alitoa tamko liloonyesha kutowajali wananchi wenzake waliokuwa hawajafurahishwa na namna rais alivyokabiliana na janga hilo.

“Acheni kupinga na kulalamika,” rais alisema. “Mpaka lini mtaendelea kulalamika?” Bolsonaro alikuwa anazungumza katika jimbo la Goias, Brazil, ambako takriban watu 9,000 walifariki.

Ni Marekani peke yake ndio ina vifo zaidi vya COVID kuliko Brazil. Kwa mujibu wa Hopkins, Marekani ina zaidi ya vifo 522,000 vya COVID-19, wakati Brazil imeripoti zaidi ya vifo 262,000.

Idara ya takwimu ya Russia imesema Ijumaa zaidi ya Warussia 200,000 waliogundulika na maambukizi ya COVID-19 wamefariki, zaidi ya mara mbili ya idadi inayotolewa na kikosi kazi cha serikali kinacho shughulikia virusi vya corona.

Idadi iliyotolewa Ijumaa na Rosstat, idara ya serikali ambayo inachapisha takwimu sio mara kwa mara, imesema ilikuwa imesajili vifo 200,432 hadi mwezi Januari. 

Takwimu hizo ni pamoja na takriban watu 70,000 waliokuwa na maambukizi ya virusi hivyo wakati wanafariki, lakini sababu kuu ya vifo vyao haijazingatia kuwa ni COVID-19.

Kwa kutumia takwimu za Rosstat, Russia itakuwa ni ya tatu yenye vifo vingi vya COVID-19 duniani, ikiifuatia Marekani na Brazil

Rosstat pia imeripoti Ijumaa kuwa Russia imesajili zaidi ya vifo 394,000 tangu kuanza kwa janga hilo hadi kufikia mwisho wa Januari kuliko katika kipindi kilichopita --- ikionyesha kuwa vifo vinavyotokana na virusi vya corona nchini humo huenda vikawa juu zaidi.

Chanzo:Dw


EmoticonEmoticon