Donald Trump Amkosoa Vikali Raisi Wa Marekani Joe Biden, Soma Hapa Aliyoyasema Katika Hotuba Yake

 

Donald Trump anasema hana mipango ya kuanzisha chaka kipya cha kisiasa, akiuambia mkutano wa wahafidhina mjini Florida kuwa hilo litagawanya kura za Warepublican.

Katika hotuba yake ya kwanza tangu Mdemocrat Joe Biden awe rais, Bw Trump pia alidokeza kuwa anaweza kugombea tena urais mwaka 2024.

Alimkosoa vikali mrithi wake, akisema kuwa sera ya Marekani imetoka kuwa " Marekani kwanza na kuwa Marekani mwisho ".

"Ninasimama mbele yenu leo kutangaza kwamba safari yetu nzuri tuliyoianza miaka minne iliyopita haijamalizika ,"alisema.

"Tumekusanyika hapa mchana huu kuzungumzia kuhusu hali ya baadae-hali ya baadae ya vuguvugu letu, hali ya baadae ya chama chetu, na hali ya baadae ya nchi yetu tunayoipenda ."

Bw Trump alipuuzilia mbali wazo lolote la kwamba ataanzisha chama kipya cha kisiasa- akielezea tetesi kwamba angefanya hivyo kama "taarifa za uzushi".

"Hilo si litakua ni jambo zuri? Ngoja tuanzishe chama kipya ili tugawe kura zetu na tusishinde kabisa ," alitania.

"Tuna chama cha Republican . Kitaungana kuliko ilivyowahi kutokea awali na kuwa imara zaidi kuliko kilivyokuwa."

Hotuba hiyo inakuja wiki mbili baada ya Bw Trump kuondolewa kesi ya mashitaka dhidi yake.


EmoticonEmoticon