Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumatano March 31

 

Tetesi za Soka Ulaya Jumatano March 31, 2021

1. Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, 27, atakuwa mlengwa wa Manchester City ikiwa viongozi wa Ligi ya Primia watashindwa kumsajili mchezaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland msimu huu. 

2. Manchester City na Chelsea zote zimembaini mshambuliaji wa Inter Milan Romelu Lukaku, 27, raia wa Ubelgiji kama mchezaji wao mbadala ikiwa zitashindwa kumsajili Haaland, 20. 

3. Man City ina inami kubwa ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway Haaland msimu huu kama mbadala wa Sergio Aguero.

4. Mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, 22, amewaambia wasimamizi wa soka wa Ufaransa kwamba hataweza kushiriki michezo ya Olimpiki mjini Tokyo, kwani anataka muda wa kutafakari hatma yake ya baadae katika klabu hiyo. PSG imepatiaofa ya mkataba mpya, huku Liverpool, Manchester City na Real Madrid zikimng'ang'ania. 

5. Mshambuliaji Lionel Messi, 33, hatahivyo, ameiambia Barcelona kumsajili Aguero, na Mwajentina mwenzake kunaashiria hitaji la msingi kuendeleza mkataba wake na klabu hiyo ya Kikatalani . 

Hata hivyo Barcelona, inaonekana kama yenye uwezekano mkubwa wa kumnyakua Aguero, ingawa klabu hiyo haijampa kipaumbele badala yake inawafuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Lyon raia wa Uholanzi, 27, Memphis Depay, Haaland wa Dortmund na Lukaku wa Inter kama vijana wadogo bado na machaguo yanayofaa zaidi.


EmoticonEmoticon