Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumatano Machi 3

Tetesi Za Soka Ulaya March 3, 2021

1. Mgombea urais wa Barcelona Joan Laporta amesema mshambuliaji nyota wa Argentina Lionel Messi, 33, ataondoka klabu hiyo ikiwa hatashinda uchaguzi wa Machi 7. Mkataba wa sasa wa Messi unamalizika msimu huu.

2. Manchester United lazima " itikise ardhi na mbingu" kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland,20, au mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe,22, anasema mlinzi wa zamani wa Red Devils, Rio Ferdinand.

3. Barca na Atletico Madrid wameagizwa kupunguza mishahara kwa kiwango kikubwa kutokana na jinsi janga la corona lilivyoathiri La Liga. 

4. Mchezaji wa kimataifa wa Wales Gareth Bale, 31, ambaye yuko Tottenham kwa mkopo ataishinikiza Real Madrid kuheshimu mwaka wa mwisho wa mkataba wake ambao malipo yake ni £600,000-kwa wiki, hata kama ataachana na mabingwa hao wa Uhispania msimu huu. 

5. Real Madrid wako tayari kumuuza mchezaji wao wa safu ya kati na nyuma Mfaransa Raphael Varane kwa Manchester United baada ya kukubali kiungo huyo aliye na umri wa miaka 27, hatasaini mkataba mpya uwanjani Bernabeu.


EmoticonEmoticon