Utajiri Wa Rapa Jay Z Umeongezeka Kwa Kasi Zaidi Kwa Mwaka 2021

 

Thamani ya Rapa wa Marekani Shawn Corey Carter maarufu Jay Z imeongezeka baada ya kuingia katika mkataba wa kuuza kampuni ya muziki inayotoa huduma mtandaoni Tidal kwa kampuni ya malipo ya simu ya Jack Dorsey kwa dau la $297 million.

Makubaliano hayo yalifanyika wiki moja baada ya rapa huyo kuuza nusu ya kampuni ya mvinyo ya Brignac Champagne kwa LVMH kwa makubaliano ya thamani ya $640 m.

Kulingana na Jarida la Forbes , utajiri wa Jay Z ulipanda kwa asilimia 40 baada ya mauzo ya kampuni hizo mbili kumfanya kuongeza thamani yake kutoka $1 b hadi $1.4 b.

Kulingna na mauzo ya huduma ya Tidal , Forbes inasema kwamba rapa huyo alijipatia faida ya $149 mbali na kuwa mwanachama wa bodi ya Square.

Chini ya mkataba huo wa Tidal, hisa za wasanii zitaendelea kumiliki kampuni hiyo huku Jay Z akimiliki kiwango kidogo.

Afisa mkuu mtendaji wa Square Jack Dorsey alingia katika mtandao wake wa twitter na kutangaza hatua hiyo.


EmoticonEmoticon