Bunge
lilikua limepanga kujadili na kupiga kura Alhamis ili kupasisha mswada wa
sheria kuhusu mageuzi kwenye idara ya polisi Marekani.
Baraza la wawakilishi la Marekani limesitisha kikao
kilichopangwa kufanyika Alhamisi baada ya polisi wa kulinda usalama wa bunge
kuonya Jumatano kuhusu uwezekano wa njama iliopangwa na kundi la wanamgambo
kuvamia jengo la bunge, tishio ambalo linakumbusha shambulizi baya lililotokea
Januari 6 mwaka huu.
Bunge lilikua limepanga kujadili na kupiga kura Alhamis ili kupasisha mswada wa sheria kuhusu mageuzi kwenye idara ya polisi.
Lakini
mshauri wa mbunge mmoja wa Democrat amesema, onyo la polisi kufuatia taarifa za
idara ya ujasusi kwamba kundi la wanamgambo ambalo halijatambulika linaweza
kutishia usalama, limechangia kubadili ratiba ya baraza la wawakilishi.
Viongozi
walisema makundi yenye itikadi kali ya mrengo wa kulia ni miongoni mwa wafuasi
wa Rais wa zamani Donald Trump, waliovamia jengo la bunge mwezi Januari
wakitaka kukwamisha zoezi la wabunge kurasimisha ushindi wa Rais Joe Biden
kufuatia uchaguzi mkuu wa Novemba mwaka jana.
March 4 ni
tarehe ambapo wapanga njama wa mrengo wa kulia waliotoa madai yasiyokua na
msingi kwamba Donald Trump alishinda uchaguzi wa Novemba 3, wanaamini kuwa ndio
siku ambapo Trump ataapishwa kuongoza kwa muhula wa pili.
Ofisi ya mwanasheria mkuu imekwisha washtaki zaidi ya watu 300 walioshiriki kwenye uvamizi wa jengo la bunge, ambapo watu watano akiwemo afisa wa polisi waliuwawa katika uvamizi huo.
EmoticonEmoticon