Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumanne April 13

 

Tetesi Za Soka Ulaya Jumanne April 13

1. Juventus wanampango wa kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Ousmane Dembele, 23, mkataba wake utakapoisha 2022.

2. Manchester United wanasita kuingia katika mazungumzo na klabu ya Borussia Dortmund ya usajili wa mshambuliaji raia wa Norway Erling Braut Haaland, 20, baada ya kushindwa kuafikiana bei nafuu kwa mchezaji mwengine wa timu hiyo, Jadon Sancho mwishoni mwa msimu uliopita. 

3. Klabu za Paris St-Germain, Real Madrid na Inter Milan zinamfuatilia winga Jesse Lingard tabla ya dirisha la usability halijafunguliwa mwishoni mwa msimu. Lingard, 28, anang'ara kwa sasa ambapo anachezea klabu ya West Hamkwa mkopo akitokeaManchester United. 

4. Arsenal wangali na nia ya kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Celtic Odsonne Edouard,23, lakini wanakabiliana na ushindani kutoka Leicester. 

5. Tottenham wanajiandaa kumsajili beki wa Bayern Munich Jerome Boateng, 32. Beki huyo wa kati ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu. 


EmoticonEmoticon