Mgogoro Wa Chini Kwa Chini Kati Ya Iran Na Israel Umefika Hatua Hatari

 

Mzozo wa muda mrefu kati ya nchi mbili za Mashariki ya Kati, Iran na Israel, unaonekana kuendelea kutokota.

Iran imelaumu Israel kwa mlipuko uliotokea na kuathiri kiwanda cha utengenezaji madini ya urani katika mtambo wa Natanz.

Israel haijasema hadharani ikiwa ndio iliyotekeleza shambulizi hilo ambalo Iran inasema ni "kitendo cha hujma" lakini vyombo vya habari vya Marekani na Israel vimenukuu maafisa waliosema kikosi cha kijasusi cha Israel nje ya nchi, Mossad ndicho kilichotekeleza shambulizi hilo.

Kwa upande wake, Iran imeapa kulipiza kisasi.

Lakini hili sio tukio pekee linaloweza kuangaziwa. Kumekuwa na mashambulizi ya kulipizana kisasi kutoka kwa pande zote mbili huku zikionesha kuwa makini kutoingia katika mgogoro wa moja kwa moja ambao uthaathiri pakubwa nchi zote mbili.

Baada ya tangulizi hiyo, je hatari zilizopo ni gani na mzozo huo unaweza kuisha vipi? Vita hivyo vya chini kwa chini vinaweza kugawanywa katika sehemu tatu.


EmoticonEmoticon