Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumatano May 05

 

Tetesi Za Soka Ulaya Jumatano May 5, 

1. Real Madrid wanamfuatilia mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling,26, ambaye anaweza kuondoka Etihad kwa kitita cha pauni milioni 75. 

2. Kocha wa Everton Carlo Ancelotti anataka kumchukua mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale, 31, anayecheza kwa mkopo Tottenham msimu huu. 

3. Chelsea wanaweza kujiunga na Manchester United na Liverpool kuwannia saini ya winga Jadon Sancho baada ya Borussia Dortmund kushusha dau la kumnasa mchezaji huyo mwenye miaka 21. 

4. Manchester United imejiunga na mahasim wa ligi ya primia Tottenham na West Ham katika kinyang'anyiro cha msajili mlinda mlango wa West Brom Sam Johnstone, 28, ikijiandaa kuondoka kwa Mhispania David de Gea, 30, msimu huu wa joto. 

5. Wakati beki mwenye umri wa miaka 34 David Luiz anaingia miezi miwili ya mwisho ya kandarasi yake na Arsenal, wawakilishi wake wameanza kutafuta kilabu kipya kwa ajili ya Mbrazili huyo. 


EmoticonEmoticon