Marekani Imepitisha Sheria Ya Dharura Kuhusiana Na Bomba La Mafuta

 

Serikali ya Marekani imepitisha sheria ya dharura siku ya Jumapili baada ya bomba kubwa la mafuta la nchini humo kushambuliwa kimtandao na genge la wahalifu linalotaka malipo.

Bomba hilo kwa kina la Colonia linabeba mapipa milioni 2.5 kila siku - sawa na 45% ya mahitaji ya mafuta ya Pwani ya Mashariki nchi hiyo na liinasambaza mafuta ya dizeli, ya petroli na mafuta ya ndege.

Wahalifu wa mtandaoni walifanya hujuma dhidi ya bomba ambalo limeshindwa kushindwa kufanya kazi tangu siku ya Ijumaa na mpaka sasa bado oparesheni ya kujaribu kurudisha huduma za bomba hilo zinaendelea.

Hali ya dharura inaruhusu mafuta kusafirishwa kwa njia ya barabara.

Jumla ya majimbo 18, zimepewa muda kidogo kusafiri mafuta ya petroli , dizeli, ya ndege na aina nyingine ya bidhaa za mafuta.

Miji hiyo ni Alabama, Arkansas, Columbia, Delaware, Florida, Georgia, Kentucky, Louisiana, Maryland, Mississippi, New Jersey, New York, North Carolina, Pennsylvania, South Carolina, Tennessee, Texas na Virginia.

Wataaamu wanasema bei ya mafuta inaweza kuongezeka kwa 2-3% Jumatatu, lakini athari itakuwa kubwa zaidi kama tatizo hili litaendelea kuwepo.

Mchambuzi wa soko huru la mafuta Gaurav Sharma ameiambia BBC kuwa kuna mafuta mengi yaliyokwama kwenye vituo vya kusafishia huko Texas.

"Labda kama wataweza kutatua tatizo hilo ifikapo Jumanne, ila wapo kwenye tatizo kubwa," alisema bwana Sharma. "Maeneo ya kwanza ambayo yatapata athari yanaweza kuwa Atlanta na Tennessee, na athari inaweza kufikaNew York."

Alisema wafanyabiashara wa mafuta wanahangaika sasa ili kufikia mahitaji ya watu kwa wakati , wakati hesabu ikipungua na mahitaji haswa ya mahitaji ya mafuta ya magari yakiongezeka baada ya wahitaji wengi wakiwa wamerudi barabarani na uchumi wa Marekani ukiwa unajaribu kurudi baada ya athari za janga la corona.


EmoticonEmoticon