Zaidi Ya Watu 30 Wauawa Kwenye Mlipuko Wa Bomu Afghanistan

 

Mlipuko huo wa bomu ulitokea karibu na shule ya wasichana katika wilaya ya Washia ya magharibi ya mji mkuu wa Afghanistan, Kabul. 

Wengi wa wanafunzi waliouawa walikuwa ni wasichana kati ya miaka 11 na 15. Haikufahamika mara moja kilichosababisha mlipuko huo. Kulikuwa na taarifa zinazopingana juu ya kilichosababisha mlipuko. 

Awali baadhi ya vyombo vya habari vya viliripoti juu ya kutokea milipuko mitatu iliyosababishwa na roketi, wakati ripoti zingine zilidokeza kuwa mlipuko huo ulisababishwa na bomu lililolipuka kutoka kwenye gari.

Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani amewalaumu wapiganaji wa kundi la Taliban kwa mashambulio hayo, amesema kundi hilo linaonyesha kuwa halina nia ya kuutatua mgogoro wa nchi hiyo kwa amani na hivyo linauhujumu mchakato wa amani, hayo ni kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu.

Hata hivyo Taliban imekana kuhusika na mashambulio hayo pia imelaani mauaji hayo yaliyowalenga raia.


EmoticonEmoticon