Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumanne June 8

 

Tetesi Za Soka Ulaya Jumanne June 8

1. Manchester United wanakaribia kufikia mkataba wa kumsajili Jadon Sancho, 21, kutoka Borussia Dortmund baada ya bei ya winga huyo wa Uingereza kushuka hadi £80m. 

2. Mshambuliaji wa Ureno Ronaldo, 36, anaelekeza darubini yake kwengine licha ya kufanya mazungumzo na Juventus kuhusu hatma yake katika klabu hiyo. Endapo Ronaldo atahama Juve, Mbrazil Gabriel Jesus ,24, wa Manchester City anapigiwa upatu kuongoza katika orodha ya wachezaji watakaochukua nafasi yake. Wengine ni mshambuliaji wa Fiorentina na Serbia, Dusan Vlahovic, 21, na Muargentina Mauro Icardi, 28, wa Paris St-Germainy. 

3. Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anataka kumsaini kiungo wa kati wa Villa na England Jack Grealish, 25, msimu huu. 

4. Chelsea wameongeza juhudi za kumsaka mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland kutoka Borussia Dortmund,"wanaamini" watafanikiwa kumpata nyota huyo , kwa mujibu wa mshambuliaji wa zamani wa Ligi ya Primia Mjerumani mwenzake Jan Aage Fjortoft. 

5. Everton wamemhoji kocha wa zamani wa Wolves Nuno Espirito Santo, 47, kuhusu uwezekano wa kumrithi Carlo Ancelotti kama meneja wa klabu hiyo baada ya Mtaliano huyo kujiunga tena na Real Madrid. 


EmoticonEmoticon