Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumatano June 09

 

Tetesi Za Soka Ulaya June 9

1. Liverpool wametangaza dau la pauni milioni 25.8 kumnunua nahodha wa Roma na kiungo wa kati wa Italia Lorenzo Pellegrini, 24, kuchukua nafasi ya mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi Georginio Wijnaldum,30. 

2. Atletico Madrid wamemtoa kiungo wa kati wa Uhispania Saul Niguez, 26, kwa Manchester City ili wampate mshambuliaji wa Ureno Bernardo Silva.

3. Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 20, anapania kujiunga na Chelsea na yuko tayari kusubiri kwa mwaka mmoja kuhamia Stamford Bridge. 

4. Juventus wanamtaka Hector Bellerin na huenda wakamuachilia tena kiungo wa kati wa Wales wa miaka 30 Aaron Ramsey katika mkataba wa kubadilishana wachezaji na Gunners. 

5. Mshambulizi wa Liverpool na Japan Takumi Minamino amehusishwa na tetesi za kurejea Southampton ambako alikuwa kwa mkopo msimu uliopita baada ya kocha wa Saints Ralph Hasenhuttl kuulizia mpango wa kiungo huyo wa miaka 26.


EmoticonEmoticon