Jarida La Forbes Lamtangaza Jeff Bezos Kurudi Kwenye Nafasi Yake Ya Kwanza Kwa Utajiri Duniani

 

Jeff Bezos, mwanzilishi wa Amazon, mtandao wa biashara, amerudi tena katika nafasi yake ya kuwa tajiri namba moja duniani, kwa mujibu wa orodha mpya iliyotolewa na Jarida la Forbes.

Hii ni baada ya hisa za kampuni yake ya Amazon kupanda 2% juu kuliko kawaida na kuingiza $3.5 Bilioni kwa siku moja.

Hivyo kwasasa Bezos ana utajiri wa $193.5 Bilioni ambapo awali alikuwa na $186 Bilioni.

Ikumbukwe, Jarida la Forbes mwishoni mwa mwezi uliopita kupitia orodha yake juu ya watu matajiri zaidi duniani, iliweza kushtua ulimwengu kwani mkuu wa LVMH Bernard Arnault alimshusha chini Bezos na kushika namba moja kwenye orodha hiyo akiwa na utajiri wa $186.3 na Bezos alikuwa na utajiri wa $186.


EmoticonEmoticon