Maafisa nchini Saudi Arabia Watoa Takwimu Ya Watakaoshirika Hijja Mwaka Huu

 

Maafisa nchini Saudi Arabia wamesema ni watu 60,000 tu watakaoruhusiwa kufanya Hija, kulingana na wavuti wa Haramain Sharifain, ambao unaripoti kutoka katika misikiti miwili mitakatifu.

Aidha taarifa hiyo inasema ni wakazi wa Saudi Arabia pekee watakaoruhusiwa kufanya Hija mwaka huu, wakiwemo wa wageni wanaoishi nchini humo.

Wavuti huo unasema kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na kusambaa kwa aina mpya za virusi ya corona kote duniani.

Mwaka jana Saudi Arabia pia ilipiga maarufuku raia kutoka mataifa mengine kufanya ibada ya Hija nchini humo ili kudhibiti virusi vya corona.

Watu takriban milioni mbili vinginevyo wangetembelea Maka na Madina msimu wa kiangazi kwa ajili ya Hija hiyo inayofanyika kila mwaka kulingana na imani ya kiislamu.

Kumekuwa na hofu kwamba Hija inaweza kufutwa kabisa.

Kwa kawaida Hija ni moja ya vipindi muhimu katika kalenda ya dini ya Kiislamu. Lakini ni raia kutoka nchi nyingine ambao tayari ni wakazi wa Saudi Arabia watakaoruhusiwa kuhudhuria Hija ya mwaka huu.